17 Aprili 2025 - 16:54
Kipindi cha Nasaha za Ulimwengu | Kwa nini Mwanadamu anafanya Kiburi wakati asili yake ni Maji Machafu?!

Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (a.s) - ABNA - IBN TV AFRIKA imeendesha na inaendeleza kipindi chake muhimu cha Nasaha za Ulimwengu. Kupitia Kipindi hiki cha "Nasaha za Ulimwengu" Sheikh Ramadhan Masemo ametoa nasaha muhimu kwa Wanadamu na Walimwengu kwa ujumla ambapo ametanguliza swali hili muhimu: Ni kwa nini Mwanadamu anafanya Kiburi wakati asili yake ni Maji Machafu?! Hutamani hata kiyatazama? Sasa kiburi cha nini?!. Kisha akasisitiza katika kunukuu maneno hayo ya Imam Ali (a.s) aliposema: "Mwanadamu unajivunia nini wakati asili yako ni maji machafu? Halafu wewe kama Mwanadamu unatembea na uchafu tumboni?! Na baada ya kufa kwako unageuka na kuwa mzoga unaotoa harufu mbaya sana!" . Sasa kwa nini ujigambe kwa mali, kwa kipaji ulichopewa, uwe na kiburi?. Yote hayo ni mambo yanayopita na tutayaacha hapa hapa duniani.

Kipindi cha Nasaha za Ulimwengu | Kwa nini Mwanadamu anafanya Kiburi wakati asili yake ni Maji Machafu?!

Your Comment

You are replying to: .
captcha